Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwan Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo ya kikazi na Maafisa Ardhi wa Mkoa wa Iringa na Manispaa ya Iringa.

Maungumzo hayo yamefanyika kwa lengo la kujadili hali ya kazi na kukumbushana Wajibu wa kila mmoja katika Utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Miongoni mwa mambo yaliyosisitizwa na Naibu Waziri huyo ni pamoja na kutenda haki kwa Wananchi juu ya masuala ya ardhi sambamba na kushughulikia kikamilifu mipango waliyojiwekea ili kuleta ufanisi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwan Kikwete akiwa katika mazungumzo na Maafisa Ardhi wa Mkoa wa Iringa na Manispaa ya Iringa.

Kikao hicho, kilifanyika mara baada ya ufungaji wa Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi yaliyofanyika katika Chuo Cha Mkwawa kilichopo Mkoani Iringa.

Baadhi ya Maafisa Ardhi Mkoa wa Iringa, wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwan Kikwete.
Habari kuu kwenye magazeti ya leo July 3, 2022    
Kiwira-Kabulo mbioni kuanza uzalishaji makaa ya mawe