Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema amebaini uwepo wa vijana wenye uwezo mkubwa wa kufanya tafiti na wanaotambua umuhimu wa mafanikio katika elimu zao ila hawana mitaji na wanahitaji kusaidiwa  kifedha na vitendea kazi.

Kufuatia hali hiyo, amesema kuna ulazima wa kubadili mifumo ya elimu nchini ili iweze kumkomboa kijana wa Kitanzania anayehitimu Chuo Kikuu badala ya kumfanya mtumwa wa ajira.

Ridhiwani amesema hayo wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Dar es salaam, ambapo amesema kuwa ili kumkomboa kijana, Sera ya Elimu nchini inapaswa kuwandaa vijana kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.

Pia, Amesema kuna dhana potofu ya kutowapa nafasi mbalimbali vijana waliohitimu vyuo mbalimbali kwa kigezo cha kukosa uzoefu, hivyo Ridhiwani amewaomba waajiri kutoa nafasi kwa vijana wajifunze na kuonyesha uwezo wao.

Ridhiwani amesema itakuwa vyemema endapo hatua za haraka zitachukuliwa dhidi ya wahitimu kwa kuwapa mitaji ili kutatua janga la vijana wasio na ajira katika jamii.

Mapinduzi Cup - Azam FC Uso Kwa Macho Na Young SC
Joshua Nassari aipongeza Serikali, aahidi ushirikiano