Mbunge wa Chalinze Mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ujumbe unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kukisema chama chake cha CCM sio wa kwake bali ni watu wenye nia mbaya ya kutaka kumchonganisha na chama chake.

Amesema kuwa maneno hayo ambayo yanasambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii yakionyesha uozo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hajaandika yeye wala kusambaza yeye kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Wana CCM wenzangu mimi kama Mbunge wa Chalinze jana kumekuwa na maneno yakisambaa kwenye mitandao ya jamii, wakinionesha kwamba mimi nimeandika maneno ambayo yana malengo yakukukisema vibaya chama changu, lakini pia ya kuonyesha uozo na ujinga ndani ya chama changu. Nataka niwaakikishie Watanzania na wanachana wenzangu hayo si maneno yangu na wala sijaandika lolote jana,”amesema Ridhiwani

 

 

Jaji Mkuu atoa angalizo kwa viongozi na wanasiasa
Trump kuhutubia kongamano la uchumi duniani

Comments

comments