Kwa mujibu wa TMZ inaelezwa kuwa vyanzo vya karibu vya wapenzi hao vimebainisha kuwa Rihanna alijifungua mapema Mei 13 huko Los Angeles na kuwa hawakuchagua kuliweka wazi suala hilo mapema.

Hii imekuwa taarifa ya mshtuko kwa mashabiki wa wapenzi hao kutokana na ukimya uliopita kabla ya Rihanna kujifungua.

Mara ya mwisho tuliwaona wawili hao Mei 9 katika wikiendi ya siku ya wakina mama duniani ambapo walionekana wakipata chakula cha jioni pamoja kwenye moja ya migahawa huko Los Angeles.

Si muda mrefu sana tangu wawili hao kuweka bayana kuwa walikuwa mbioni kupata mtoto, ambapo mapema mwezi Januari, walizianika picha za ujauzito huo zilizoibua gumzo kubwa kote duniani.

Huku kundi kubwa la mashabiki wakionyesha kufurahishwa na nyota hao kufikia uamuzi wa kupata mtoto.

Katika kipindi chote cha ujauzito wa Rihanna alionekana kuwavutia wengi kutokana na mfumo wa maisha yake ulivyobadilika huku kila mara muonekano wake ukipambwa na mitindo mbali mbali ya mavazi ya ujauzito.

Kipindi cha mwisho kuelekea kumkaribisha mtoto wao wa kwanza, rapa A$AP ambaye ndio baba wa mtoto huyo alikamatwa mwezi uliopita, katika mkasa wa kushtukiza punde wakati akishuka kwenye ndege katika uwanja wa Lax, walipokuwa wakitokea huko Barbados walikokwenda katika likizo fupi.

Licha ya kupitia misukosuko kadhaa, wawili hao waliendelea kuonekana kushikamana katika kipindi chote hadi kufikia wakati ambao wamebarikiwa kumkaribisha mtoto wao wa kwanza.

Habari Kuu katika magazeti ya leo Mei 19, 2022
Kauli ya Magufuli yajirudia kwa Samia