Ripoti ya Polisi kuhusu tukio la mwanafunzi wa kiume katika shule moja ya Kikatoliki nchini Uingereza kumuua kwa kumchoma kisu mwalimu ndani ya darasa, imebainisha kuwa alifanya hivyo baada ya kukasirishwa na kitendo cha mwalimu huyo kumkatalia kuacha kusoma somo lake.

mwanafunzi-na-mwalimu

Will Cornick (kushoto) na mwalimu Ann Maguire

Mwanafunzi huyo aliyetajwa kwa jina la Will Cornick, alimuua mwalimu Ann Maguire (61) mbele ya wanafunzi wa darasa hilo Aprili 2014.

Mwalimu huyo raia wa Hispania alikuwa najiandaa kustaafu kazi yake na kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya mapumziko baada ya kutumikia kwa miaka mingi katika “Corpus Christi Catholic College.”

Ripoti ya polisi iliyochapishwa mwanzoni mwa wiki hii imeeleza kuwa hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kutabiri tukio hilo isipokuwa mtendaji mwenyewe, hivyo hakuna mtu anayepaswa kujibu zaidi ya Cornick mwenyewe.

Kijana huyo anadaiwa kuandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akitishia kumuua mwalimu huyo.

Cornick yuko gerezani akikabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 20 kwa mauaji ya mwalimu Ann.

Live: Uchaguzi wa Rais Marekani 2016, Trump & Clinton
West Ham United Kubisha Hodi Stamford Bridge