Imebainika kuwa mcheza Tenisi anaeshika namba nne kwa ubora duniani upande wa wanaume Roger Federer, atakuwa nje uwanja kwa mwaka wote wa 2020 baada ya kufanyiwa upasuaji mwingine wa goti la kulia.

Federer ambaye ni bingwa mara 20 wa mataji ya Grand Slam, mwezi wa Februari mwaka huu alifanyiwa upasuaji wa kwanza na akaendelea kupata matibabu, na sasa amefanyiwa upasuaji wapili ambao utamuweka nje kwa zaidi ya miezi sita ijayo.

“Tutakutana tena kwenye ulingo wa tenisi mwanzoni mwa mwaka 2021 katika misimu ya awali” amesema Federer ambaye ni raia wa Uswisi.

Federer hajacheza mchezo wowote rasmi tangu alipopoteza nusu fainali ya mashindano ya Australia Open mwezi wa kwanza 2020.

Mchezaji huyo amekuwa na mwendelezo wa majeruhi ambapo mwaka 2016 alikosa asilimia kubwa ya michezo kutokana na majeruhi kama hayo ya goti ingawa aliporudi akashinda Australia Open na Wimbledon.

Michezo yote Tenisi imesimama tangu mwezi Machi mwaka huu kutokana na janga la virusi vya Corona.

Maamuzi ya TFF yaikuna Mtibwa Sugar
Tetesi: Chelsea yasaliamu amri, yamgeukia Havertz