Taarifa za wanaanga zinasema kuwa roketi iliyorushwa na kampuni ya uvumbuzi wa anga za juu ya bilionea Elon Musk inakaribia kugonga ndani ya mwezi na kulipuka.

Chombo kinachosaidia roketi kulipuka kwa Falcon 9 kilikwenda katika anga za juu mwaka 2015, lakini baada ya kukamilisha safari yake, hakikuwa na mafuta ya kutosha ya kukirejesha duniania na badala yake kilibakia katika anga za juu.

Mtaalamu wa masuala ya anga za juu Jonathan McDowell amelimbia shirika la habari la BBC kuwa itakuwa mara ya kwanza kwa roketi isiyoongozwa kugongana na mwezi lakini anasema athari yake itakuwa ndogo.

Roketi hiyo iliachwa katika obit ya juu miaka saba iliyopita baada ya kukamilisha kazi ya kutuma setilaiti ya hali ya hewa katika safari ya maili milioni.

Ilikuwa ni sehemu ya mpango wa uvumbuzi wa anga za juu wa Musk-SpaceX, ambayo ni kampuni ya kibinafsi ambayo lengo lake kuu ni kuwawezesha binadamu kuishi katika sayari nyingine.

Mjasiriamali Elon Musk ametangaza mpango wake wa kuunda makao ya binadamu katika sayari ya Mirihi (Mars kwa Kiingereza), ingawa wanaotaka kunufaika watahitajika kulipa pesa nyingi.

Musk, aliyeanzisha kampuni ya kibinafsi ya usafiri wa anga za juu kwa jina SpaceX, alitangaza mpango huo katika kongamano la kimataifa la wataalamu wa anga za juu (IAC) mjini Guadalajara, Mexico, siku ya Jumanne.

Harmonize aitangaza siku yake
Ahmed Ally: Atakaecheka mwisho ndo atacheka zaidi