Rapa mwenye mashairi yanayoacha gumzo mitaani, Roma Mkatoliki ambaye hivi karibuni alitangaza ujio wake mpya wa ngoma aliyoibatiza jina la ‘Kaa Tayari’, ametaja siku rasmi atakayoiachia video na audio ya wimbo huo unaosubiriwa kwa kiu na mashabiki wake.

Akizungumza na Dar24, Rapa huyo amesema kuwa wimbo huo uliopikwa ndani ya Tongwe Records, tayari umeshaandaliwa video kali iliyoongozwa na Nick Dizzo na kwamba mzigo wote utaachiwa kwa pamoja saa chache baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Kwenye ‘Kaa Tayari’ tumeshafanya video na tumeifanya na Nick Dizzo, kwahiyo for the first time tunaachia audio na video kwa pamoja. Na tunaviachia punde tu mwezi utakapoonekana. Yaani mwezi ukionekana sasa hivi basi muda huohuo napandisha link ya video na audio,” Roma ameiambia Dar24.

Amesema aliamua kusubiri mwezi wa Ramadhani upite kutokana na heshima yake kwa kipindi hiki Kitakatifu kwa waumini wa dini ya kiislamu.

Ingawa matarajio ya wengi ni kutaka kumsikia Roma akipitia matukio ya utumbuaji majipu ya Rais John Magufuli na serikali yake pamoja na mambo mengine, msanii huyo amesema kuwa hiyo anaiacha kama surprise kwa mashabiki.

“Sasa watu wanachoexpect ni kwamba labda Roma aje afanye kitu fulani, lakini msanii mzuri ni yule ambaye anafanya kitu ambacho watu hawaexpect. Kwahiyo wakati mwingine unaweza kuachia jiwe ambalo watu hawalitegemei. Ndio maana kwenye ‘Kaa Tayari’ tukawaambia hapana, ili iwe exclusive inabidi wasubiri wasikilize Roma ameimba nini..” alisema.

Mwaka jana, Roma alikumbwa na dhahma ya kufungiwa wimbo wake wa ‘Viva’ ambao ulipokelewa kwa nguvu na mtaa, lakini Mamlaka husika ziliuondoa kutokana na maudhui yake.

Baada ya ‘Viva’ kutumbuliwa, Msanii huyo aliachia wimbo wa mapenzi alioubatiza jina la ‘Mtoto wa Kigogo’, na sasa anakuja na Kaa Tayari ambayo haitabiriki kama italiacha mbali jina la Rais Magufuli ama operesheni ya tumbua majipu na matokeo yake.

Maandamano Dhidi ya Kupinga Mauaji Kenya
Makocha Wa Hispania Kumchambua Mmoja Mmoja Azam FC