Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amejikuta kwenye wakati mgumu kufuatia kauli aliyotoa baada ya mtanange wa jana ulioshuhudia timu yake ikibanwa na Iceland kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Ronaldo waliishambulia timu ya taifa ya Iceland, kwa kusema ilishindwa kucheza soka na badala yake ikafanya kazi ya kuzuia wakato wote, hatua hatua mbayo anaamini iliwanyima Ureno kucheza soka lao na kupata ushinid.

Kauli hiyo ya Ronaldo imeonyesha dhahir anaamini katika kupata matokeo chanya na si vinginevyo.

Kutokana na uchanga wa taifa la Iceland katika nyanja ya michezo barani Ulaya, Ronaldo alipaswa kuwapongeza badala ya kuwatolea maneno ya kejeli….baada ya mchezo wa jana, Ronaldo alikaririwa akisema.

“Iceland walikuwa na lengo la kujilinda tu…walipata nafasi mbili lakini hata hawakujaribu kufunga.

Baada ya sare waliyopata walisherehekea mithili wamechukua ubingwa wa Euro au kitu gani sijui, hiyo ni akili ndogo. Na ndiyo maana hawatafanya chochote katika michunao hii.”

Wachambuzi wa masuala ya soka wamesema kitendo cha mchezaji wa aina yake kuzungumza maneno yasiyo ya kimichezo dhidi ya Iceland katika mchezo wa jana, ambapo timu yake ya Ureno ilibanwa mbavu na kutoka sare ya bao 1-1 katika michuano ya Euro mchezo wa kundi F hakikuwa cha kiungwana.

Wakati huo huo mshabiki wa soka duniani wamemshambulia Ronaldo katika mitandao ya kijamii kwa kuandika maneno ya kejeli dhidi yake, kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Video: Solo Thang amkingia kifua Jay Mo
Simba Waendelea Kumsaka Kocha Kimya Kimya