Makamu wa Rais nchini Kenya William Ruto amesema yuko tayari kumaliza mvutano uliojitokeza kati yake na Rais Uhuru Kenyatta bila ya masharti yoyote.

Hatua hiyo imejili baada ya Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya kuwataka viongozi hao wamalize tofauti zao.

Uhasama kati yao umesababisha hali ya hofu katika taifa la Kenya ambalo linakaribia kufanya uchaguzi na lenye historia ya machafuko kila wakati uchaguzi unapoandaliwa.

Mwezi uliopita Rais Kenyatta alimhimiza Makamu wake kujiuzulu iwapo haridhishwi na utendaji kazi wa serikali. Kiyume chake  Ruto aliapa kwamba hatojiuzulu kwani hatua hiyo ingemwonesha kuwa mwanasiasa  mwoga na msaliti.

Ruto amekua wa kwanza kuitikia  wito wa maaskofu wa kanisa katoliki wa kufikia maridhiano.

“Mimi niko tayari. Hawa Maaskofu wamesema wanataka kuniweka pamoja na rais. Mimi niko tayari bila masharti. Kwa sababu mimi ninamuheshimu rais yeye ni kiongozi wangu,” amesema Ruto

Maaskofu 23 wa jimbo la Nyeri huenda wakawa suluhu ya mgogoro huo kupitia mkutano wa kanisa katoliki waliofanya chini ya mwavuli wa Kongamano la Maaskofu.

Muongozo wa mpango wa kuwapanga wamachinga
Kilio cha wana Mahembe chasikika