Kikosi cha wachezaji 20 na Viongozi 13 wa timu ya Ruvu Shooting ya Pwani kimeondoka mapema Alfajiri March 30, kuelekea Jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi, April 1, 2017 katika uwanja wa Sokoine Jijini humo.

Kikosi hicho chini ya uongozi wa Luteni wa Jeshi, Stanley Chahe, Afisa Habari na Mahusiano, Masau Bwire, Kocha Mkuu Malale Hamsini, baada ya mchezo huo, kitaelekea Kyela ambapo kitacheza mchezo wa Kirafiki April 2, 2017.

Baada ya hapo, kikosi kitarejea nyumbani, Mabatini kujiandaa na mchezo dhidi ya Majimaji utakaochezwa uwanja wa Mabatini, April 15, 2017.

Sakata la makontena lageuka kaa la moto
Magazeti ya Tanzania leo Machi 30, 2017