Gazeti la Daily Telegraph, limemtia matatani kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Sam Allardyce kwa madai alizungumzia njia zisizo halali za Uhamisho wa Wachezaji.

Gazeti hilo limechapisha habari kuwa waandishi wa habari waliojifanya wafanyabiashara, walizungumza na Allardyce maarufu kama Big Sam, ambae alikiri inawezekana kuizunguka sheria ya chama cha soka nchini Uingereza (FA) ya Mwaka 2008 ya kuzuia mchezaji kuwa mali ya mmiliki mwingine Kibiashara mbali ya Klabu yake.

Ripoti ya Daily Telegraph imedai kuwa Big Sam alienda mbali zaidi na kufikia hatua ya kumdhihaki kocha wa Uingereza aliyemtangulia (Roy Hogson) na haikuishia hapo bali aliinanga tena FA kwa kusema inajali kutengeneza fedha na sio jambo lingine lolote.

Sam Allardyce was caught in a sting by The Telegraph newspaperPicha iliyotokana na sehemu ya Video iliyorekodiwa wakati wa mkutano na wafanyabiadhara feki

Gazeti hilo pia limerusha mtandaoni video inayoonyesha mkutano huo na wafanyabiadhara feki wakati Big Sam akimponda Hodgson na kuikandia FA.

FA wamethibitisha kuwepo kwa sakata hilo na tayari wameutaka uongozi wa gazeti la Daily Telegraph kuwapa ukweli wote kuhusu Mkutano huo.

Inasemekana Allardyce hajasema chochote mara baada ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo.

Majaliwa aiweka RUBADA kikaangoni, Asema inaendeshwa kwa ubabaishaji
Video: JPM afichua madudu Bandari ya Dar es salaam