Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mamluki na wasaliti ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni moja kati ya vyanzo vya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Mama Samia aliyasema hayo hivi karibuni Jijini Tanga, alipofanya mkutano na wenyeviti wa Jumuiya ya mbalimbali za CCM, Makatibu na wajumbe wa kamati za wilaya zinazounda mkoa huo, kikao kilichofanyika kwenye makao makuu ya chama hicho jijini humo.

Alisema kuwa mamluki hao na wasaliti walikuwa wakijifanya wana CCM huku wakiwapigia debe kimyakimya wagombea wa upinzani, hivyo kuzua mgongano mkubwa wa maslahi uliozua mgogoro wa Zanzibar. Aliwataka makada hao kulichukulia suala la mgogoro wa Zanzibar kama sehemu ya fundisho kwao.

“Suala la Zanzibar kwa sasa liwe sehemu ya fundisho tosha kwa wanachama wa CCM, kwa kiasi kikubwa limesababishwa na kutowajibika kwa wanachama, hali hiyo ndiyo imetulazimu kufika hapa tulipo,” Mama Samia ananukuliwa.

Aliwataka wanachama hao kuungana kukisafisha chama hicho na kuwaondoa wasaliti na wazembe ili kiweze kusonga mbele na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Maagufuli.

Wassira amchana January Makamba
Kutoka Zenji: Soka La Zenji Bado Ni 'Kitahanani', Limeanza Kama Masihara hadi mahakamani