Ujumbe wa Wizara ya Madini ukijumuisha Viongozi na Wataalam kutoka Taasisi zake umekutana na wawekezaji wa Sekta ya Madini kutoka nchi mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika sekta hiyo nchini.

Kampuni hizo ni Elves Graphite ya Korea Kusini ambayo ina nia ya kuwekeza kwenye uchimbaji na ununuzi wa madini ya kinywe yaani graphite wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi, Kampuni ya WorldKare ya Dubai ambayo inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya usalama migodini kampuni ya MCF Conseil ya Ufaransa na kampuni ya Design Fabrication India inayoshughulika na ukataji wa bidhaa mbalimbali.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Kampuni ya Elves Graphite Lee Jae-Jin ameeleza kuwa kampuni imepanga kuwekeza Tanzania kutokana na uhakika wa kupata walaji wa madini hayo kutoka kampuni mbalimbali nchini Korea Kusini ikiwemo ya Samsung inayotengeneza bidhaa za teknolojia.

Kwa upande wa kampuni ya MCF Conseil ya Ufaransa chini ya Rais wa kampuni hiyo Sabine Moutier, amesema kuwa wanatarajia kufanya biashara ya ununuzi wa dhahabu iliyosafishwa kutoka viwanda vya ndani. Kampuni hiyo imeomba kupatiwa taratibu za biashara hiyo ili kuweka waweze kujipanga zaidi kabla ya kuanza rasmi biashara hiyo.

Hivi karibuni, Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko ameleezea mwelekeo wa Serikali kwa siku za usoni wa kuzuia usafirishaji wa dhahabu ghafi hadi pale zitakapokuwa zimesafishwa kupitia viwanda vyake vya ndani vilivyoanzishwa katika mikoa ya Mwanza, Geita na Dodoma ambavyo vina uwezo wa kusafisha dhahabu kwa ubora wa viwango vya kimataifa.
Kwa mujibu wa Wizara ya Madini, kutokana na kuanzishwa kwa viwanda vitatu vya kusafisha dhahabu ni dhahiri kuwa, dhahabu inayozalishwa Tanzania inaweza kusafishwa kupitia viwanda vyake hivyo kikiwemo kiwanda kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati cha Mwanza Precious Metals Refinery Limited (MMPR) chenye uwezo wa kusafisha kilo 480 za dhahabu kwa siku katika ubora wa kiwango cha Kimataifa cha asilimia 999.9.

Aidha, ujenzi wa viwanda vya kusafisha dhahabu nchini ni matokeo ya jitihada za Serikali kuhamasisha masuala ya uongezaji

Bima ya afya kwa wote kuelekea miaka 60 ya Uhuru Tanzania
Mguto aibuka sakata la GSM