Meneja wa klabu ya Besiktas, Senol Gunes ameonyesha kutokau tayari kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool, Mario Balotelli.

Gunes, amesema hana mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kutokana na kumfahamu vilivyo na hakuwahi kusikia sifa njema kutoka kwake.

Kauli ya Gunes, imekwenda kinyume na ile ya rais wa klabu hiyo Fikret Orman aliyoitoa juma lililopita, kwa kusema anatamani kumuona Balotelli akitua Vodafone Arena katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

“Balotelli hayupo katika mipango yangu,” Alisema meneja huyo.

“Sina mipango wala matarajio ya kuwa na mshambuliaji kwa sasa, kutokana na kuwamini waliopo kikosini, na hata kama itatokea ninafanya usajili, basi haitokua kwa Balotelli.

“Sikuwahi kusikia mazuri ya mshambuliaji huyu tangu nilipomfahamu, zaidi ya kusikia vihoja na vituko.” Alisisitiza Gunes

Balotelli amekua katika mawindo ya klabu atakayoitumikia msimu ujao wa ligi baada ya meneja wa Liverpool  JurgenKlopp, kumueleza wazi, hayupo katika mipango yake.

Schalke 04 Wakanusha Taarifa Za Leroy Sane
Claudio Ranieri: Nimechoshwa Na Taarifa Za Riyad Mahrez