Usiku wa kuamkia hii leo huenda ukaingia katika kumbukumbu za mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Aguero, baada ya kushindwa kuinusuru timu yake ya taifa ya Argentina katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi.

Aguero aliahidi kupambana kadri awezavyo mara baada ya kikosi cha Argentina kuambulia matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Peru mwishoni mwa juma lililopita, lakini ilikua tofauti walipokutana na Paraguay mjini Cordoba.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alijikuta akikosa mkwaju wa penati katika mchezo huo muhimu ambao ulistahili kushuhudia kikosi cha Edgardo Bauza kikichomoza na ushindi lakini mambo yalikwenda mrama.

Aguero alicheza kwa dakika zote 90 na walinzi wa Paraguay waliokuwa makini kumkaba ili asiwaletee madhara langoni mwao, na mwishowe mipango hiyo ilifanikiwa kwa asilimia 100.

Kufungwa katika mchezo huo kunaendelea kuifanya Argentina kushika nafasi ya tano katika msimamo wa kundi la kusini mwa bara ya Amerika kusini, huku timu zote za ukanda huo zikiwa zimecheza michezo 10.

Aguero anatarajiwa kurejea Uingereza akiwa na kumbukumbu za kushindwa kuibeba Argentina katika mchezo muhimu, huku mtihani mwingine ukimsubiri mwishoni mwa juma hili pale Man City itakapokua mgeni wa Everton katika uwanja wa Goodison Park.

Nyerere chimbuko la Ukombozi Afrika
Rais Magufuli aagiza viongozi kurudisha fedha za mwaliko wa Mwenge, awataka kutohudhuria