Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwa kwenye ziara yake ya kutembelea wilaya mpya jijini Dares salaam akianza na kigamboni amesema mchakato wa kuajiri walimu 4000 wa masomo ya sayansi na hisabati unaendelea chini ya ofisi ya Utumishi na muda wowote kutoka sasa mchakato utakapokamilika majina hayo yatatolewa na walimu kuajiliwa.

Hivi karibuni, Wizara ya Elimu iliwataka wahitimu wa ualimu katika masomo  ya sayansi na hisabati kutuma taarifa zao (CV) ili izihakiki taarifa zao kabla ya kutoa ajira, mchakato ambao tayari umekamilika na majina yalitumwa katika Wizara ya Utumishi.

Katika hatua nyingine Majaliwa ameagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mkoa wa Dar es salaam kufuta malipo ya posho zote za vikao visivyo rasmi pamoja na fedha za vitafunwa, fedha hizo zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo ametaka zoezi hilo lianze mapema mwaka huu 2017.

Pia ametoa siku 10 kwa watumishi waliohamishwa kutoka wilaya ya Temeke kwenda Wilaya ya Kigamboni wawe wameripoti katika wilaya hiyo ya kigamboni vinginevyo mamlaka husika kuwafuta kazi wasiwe tena kwenye ajira za serikali.

Ligi Kuu Soka Ya Wanawake Tanzania Bara Kuendelea
Asha Baraka: Najipanga kuwaachia vijana muziki wa dansi na kuingia kwenye siasa