Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema Wananchi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile vituo vya afya, madarasa, maji, umeme na barabara na kwamba kwasasa mbali na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo pia wanalenga kutatua shinda nyingine za Wananchi.

Ameyasema hayo, Kufuatia ombi la ombi la Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza kutaka Mbalizi kupandishwa hadhi na kuwa halmashauri ya mji, ambapo Rais amesema Serikali haina mpango wa aina hiyo na kwamba kwasasa imejielekeza katika utatuzi wa shida za wananchi

Ombi hilo, lilitolewa na Mbunge huyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suhulu Hassan ambaye yuko Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi iliyoanza hii leo Agosti 5, 2022 baada ya kusimama na kuwasalimia wananchi wa Mbalizi.

Akiongea mbele ya Rais, Njeza alisema anaomba mji wa Mbalizi upandishwe hadhi na kuwa Halmashauri ya mji, kwa madai kuwa hatua hiyo itasaidia kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi wa maeneo hayo kutokana na hali ya kijiografia kutokuwa rafiki kwa baadhi ya maeneo.

Akijibu hoja hiyo, Rais Samia amesema, “Wananchi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile vituo vya afya, madarasa, maji, umeme na barabara, hivyo Serikali haitawezekana kufanya yote kwa wakati mmoja.”

Rais Samia yupo Mkoani Mbeya katika ziara ya kikazi ya kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ile ya afya na ujenzi wa barabara.

Okwa atamba kufanya makubwa Simba SC
Edo Kumwembe: Young Africans inanipa homa