Polisi nchini Uganda wamevunja tamasha la wapenzi wa jinsia moja lililokuwa limeandaliwa katika mji wa entebe nchini humo.

Mapenzi ya watu wa jinsia moja yalidhuiliwa nchini Uganda chini ya sheria za ukoloni katika kifungu kinachokataza mtu kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Waziri wa sheria nchini Uganda Simon Lokodo mwezi uliopita alisema shughuli zote za wapenzi wa jinsia moja ni haramu na kinyume na tamaduni za watu wa Uganda

Polisi ilipiga marufuku mkutano wa wapenzi wa jinsia moja katika klabu moja ya usiku mjini Kampala wiki chache zilizopita.

Hata hivyo mwanaharakati wa kupigania haki za wapenzi ya jinsia moja nchini Uganda alisema kuwa watu wenye wapenzi wa jinsia moja wanastahili kuendelea na shughuli zao kama kawaida kama watahitaji kufanya hivyo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Frank Mugisha alisema kuwa ”jamii ya LGBT itaendelea kufanya mikutano yao kama ilivyoruhusiwa kikatiba bila pingamizi lolote”

Waziri wa sheria nchini Uganda amesema kuwa serikali yake haitawafumbia macho wale wanaoshabikia wapenzi wa jinsia moja na kujaribu kusambaza harakati zao alizoziita haramu nchini humo.

”Katika jamii yetu maswala ya mapenzi huwa ni ya siri mno, iweje kwa sasa maswala ya ngono yanawekewa gwaride ? tutapambana na mtu yeyote atakaye jaribu kuchochea ama hata kufadhili na kupigia debe swala la wapenzi wa jinsia moja”Alisema Lokodo.

Viongozi wa Vyama vya Siasa Watakiwa kuwa wazalendo
Mahakama Nchini Gabon Yamtangaza Ali Bongo kuwa Mshindi wa kiti cha Urais