Tatizo la Ukosefu wa Madaktari Bingwa hususan katika maeneo ya mikoa ya pembezoni linaweza kuwa historia au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa baada ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kuahidi kuwapeleka madaktari hao mwaka huu.

Ahadi hiyo ya serikali imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Dk. Hamis Kigwangalla alipofanya ziara ya kushtukiza katika hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma pamoja na kituo cha afya cha Mjimwema kilichopo mjini Songea mkoani humo.

Dk. Kigwangalla ameahidi kuwa Serikali itaanza kusambaza madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali katika maeneo ya pembezoni kuanzia Julai mwaka huu.

Aidha, Naibu Waziri huyo amewataka wakazi na viongozi wa mikoa hiyo kuhakikisha wanatengeneza mazingira rafiki yatakayowavutia madaktari hao kufanya kazi katika maeneo hayo.

Naye Mkuu mkoa wa Ruvuma, Said  Mwambungu alimwambia Dk. Kigwangalla kuwa wanaendelea kufanya jitihada za kuboresha huduma za afya katika vituo vya afya vilivyoko katika maeneo yao na kwamba wameridhishwa na mtindo wa kufanya ziara za kushtukiza.

Rais wa Pakistan apiga marufuku 'Valentine's Day', aeleza sababu za kuitosa
Utashangaa kilichomtokea Mbwa Kichaa aliyemng'ata Polisi