Wizara ya Afya imetolea ufafanuzi zaidi juu ya matumizi ya barakoa kwa wanafunzi, ambapo imeelekeza zitumike katika mazingira ya msongamano ili kudhibiti maambukizi ya Corona.

Wanafunzi walio chini ya miaka 8 na wote wenye matatizo ya kiafya ikiwemo Pumu, matatizo ya moyo na Selimundu wametakiwa kutotumia kabisa barakoa.

Serikali imeelekeza walio na matatizo ya figo, Kisukari, Shinikizo la damu na walio na unene mkubwa kuvaa barakoa huku wakiwa katika uangalizi wa karibu.

Aidha, Wanafunzi wametakiwa wasivae barakoa wakati wa michezo na pale wanapofanya mazoezi ikiwemo wanapokimbia mchakamchaka.

Magaidi wauawa katika shambulizi Pakistan
JPM atoa siku saba kufutwa hati za mmiliki wa ardhi asiye mtanzania