Serikali ya Mkoani Geita imegharamia maziko ya kijana, Shinje Charles aliyefariki kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) huku ikitoa siku saba (7) kuhakikisha upelelezi unafanyika kuhusu tukio hilo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mwili nwa marehemu huyo kukaa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita kwa siku kumi  na moja (11)  baada ya ndugu kugoma kuuzika wakishinikiza ufanyike uchunguzi wa kina.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga na kamati ya ulinzi na usalama ilifika kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM kuangalia maeneo yanakosadikiwa kuwa kijana huyo alianguka kwenye  shimo  liilokuwa limechimbwa.

Aidha, Mkuu wa mkoa wA Geita amesema kuwa wao kama serikali wamechukua uamuzi wa kuzika mwili huo  kutokana na kukaa muda mrefu bila kuzikwa na kwamba upelelezi wa kifo hicho unaendelea.

Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Geita, Joseph Msukuma amesema hatua ya serikali kuzika imekuja baada ya GGM kusema wako tayari kutoa jeneza na gari na vitu vingine vichangiwe na wananch

“Kumekuwa na mvutano mkali GGM  wanasema wako tayari kuchangia jeneza na gari tulichokifanya namshukuru DC Geita waamesema wapeleke gari lao na jeneza hivyo tulichokifanya DC ametoa laki mbili na mimi kama mbunge nimetoa laki sita,”amesema Msukuma.

Hata hivyo kijana, Shinje Charles alifariki August 21 mwaka huu baada ya kuingia mgodini kuchukua mawe ya dhahabu maarufu, Magwangala.

Breaking News: Mahakama yabatilisha uchaguzi wa urais Kenya, yaagiza kufanyika upya
Video: Majambazi wanne wauawa Dar