Serikali imetoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia ya kuuza ovyo ardhi huku wao wakibaki na eneo dogo lisilokuwa na rutuba na halitosherezi matumizi ya familia zao katika siku za baadaye.

Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwenye sherehe za kilele cha maonyesho ya Nane Nane kwa Kanda ya Magharibi yaliyofanyika katika Viwanja vya Fatuma Mwasa mkoani humo.

Amesema kuwa kutokana na Mkoa wa Tabora kuanza kufunga kwa kasi miundo mbinu mbalimbali kama vile usafiri wa uhakika wa anga, kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria, ujenzi wa reli ya kisasa na barabara za lami zinaongeza fursa ya watu mbalimbali kwenda mkoani humo kwa shughuli mbalmbali.

Aidha, amesema kuwa watu hao wanaweza wakajitokeza na kuanza kuwarubuni wakazi ili wawauzie ardhi zao hata kwa bei ambayo hailingani na eneo husika huku wenyewe wakipata fedha kidogo ambazo hazimsaidii kujiendeleza bali kuendelea kuwa maskini.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa thamani ya ardhi inaongezeka kila siku na watu wanaohitaji wanaongezeka hivyo ni vema wakawa makini kabla ya kufanya maaumuzi  ya kuuza vipande vyao vya ardhi ili wasije wakajuta mara fedha walizolipwa zitakapokuwa zimekwisha.

 

Video: Ruge azungumza haya baada ya kukutana na Makonda, Jukwaa la Wahariri
Rafael Benitez: Sifurahishwi Na Usajili Wa Newcastle Utd