Aliyekuwa Rais wa Somalia Mohamed Abdullah Farmajo amekubali kushindwa katika Uchaguzi uliofanywa na wabunge wa nchi hiyo hapo jana na kumfanya aliyekua Rais miaka ya nyuma Sheikh Mohamud kuwa Rais mpya.

Uchaguzi huo ulishirikisha wabunge 328 pekee kutokana na suala la ukosefu wa usalama ambao huenda lingeathiri uchaguzi huo , huku mbunge mmoja akikosa kupiga kura.

Wabunge watatu waliripotiwa kuharibu kura zao, Bwana Mohamud alipokea kura 214 , akimshinda Farmajo ambaye alipata kura 110.

Alimshinda rais aliyepo madarakani Mohammed Abdullahi Farmajo ambaye amekuwa akihudumu tangu 2017.

Matokeo hayo yanaadhimisha kurudi kwa Hassan Sheikh Mohamud , aliyehudumu kati ya 2012 hadi 2017 kabla ya kushindwa na Farmajo.

Uchaguzi huo ambao ulikuwa na ushindani mkali na ambao uliingia katika raundi ya tatu – ulicheleweshwa kwa takriban miezi 15 kutokana na vita na masuala ya usalama.

Bwana Mohamud aliapishwa muda mfupi baada ya matokeo ya mwisho kutangazwa , na kuwafanya wafuasi wake katika mji huo kumpongeza mbali na kufyatua risasi hewani na atahudumu kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Katika uchaguzi huo wa Jumapili , mamia ya wabunge walipiga kura zao katika anga moja ya ndege katika mji mkuu wa Mogadishu.

Milipuko ilisikika karibu na eneo hilo huku uchaguzi ukiendelea lakini maafisa wa polisi wanasema kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Akiwa rais mpya, bwana Mohamud atalazimika kukabiliana na athari za ukame ambapo Umoja wa mataifa unasema kwamba takriban raia milioni 3.5 wako hatarini kukumbwa na kiangazi cha kiwango cha juu.

Lakini jukumu kuu analokabiliana nalo ni kukomboa eneo kubwa la taifa hilo ambalo lipo chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Alshabab.

Mwanasiasa aliyetekwa apatikana akiwa amefumbwa macho
Habari kuu kwenye magazeti ya Leo Mei 16, 2022