Makamu mwenyekiti  wa CCM (Zanzibar), Dkt. Ali Mohamed Shein,amesema kuwa hakuna mtu yeyote mwenye ubavu kutoka Umoja wa Mataifa au Mahakama ya Kimataifa atakayeweza kumuondoa madarakani na CCM itaendelea kushika hatamu hadi pale uchaguzi mwingine utakapofanyika.

Ameyasema hayo katoka ufungji wa Kampeni za CCM zilizofanyika katika uwanja wa shule ya Skuli Sekondari Fuoni, amesema kuwa inasghangaza kuendelea kusikia kutoka kwa wapinzani wa CCM,kuwaahidi wanachama wao kuwa wanasubiri Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa imuondoe madarakani jambo ambalo haliwezekani na halitotokea.

Amesema kuwa Umoja wa Mataifa hauwezi kuiingilia Zanzibar nchi iliyofanya uchaguzi wake kwa kuzingatia Demokrasia na haitakuwa rahisi kutka kwa mitizamo hiyo kwa vile mataifa hayo yanatambua kilichofanyika ni halali.

“Nchi hii haitoki na wataiona hivi hakuna mtu hata mmoja wa kunitoa si Umoja wa Mataifa wala Mahakama ya The Hague, watafute jingine la kuwadanganya wanachama wao, hapa ni mpaka 2020 wasikudanganyeni,” amesema Shein.

Hata hivyo Shein amesema kuwa ili CCM izidi kuwa na nguvu zaidi laima jimbo hilo lirudi katika mikono ya Chama Cha Mapinduzi kwani hakuna mwenye uwezo wa kuiondoa.

Video: Serikali yatoa sh. bilioni 1.4 ujenzi wa Hospitali Njombe
'Serikali imeanza kulipa madeni ya watumishi' - Majaliwa