Umeshawahi kufikiria kurudi darasani kusoma ili tu ufahamu kitu ili uweze kupata michongo mingine ya mbali zadi, au bado unafikiria umri umekwenda bora utafute pesa na siyo kurudi darasani kama unawaza hivyo basi hauwezi kuwa msafara mmoja na Zuwena Mohamed ‘Shilole’

Bi dada alianza kwa kuwa mama ntilie kabla ya kujulikana kama muigizaji lakini pia mrembo wa kupendezesha video mwisho akageukia uimbaji ambako mpaka sasa anaonekana kufanya poa.

Muite Shilole Mtoto wa Igunga anajulikana kwa drama nyingi sana ambazo nyingine alionekana kama anaigiza likiwemo suala la kutojua kiingereza yeye pamoja na aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda.

Unaikumbuka ”hello i lav u, Tanzania is my country? ambayo ilipokelewa kwa hisia tofauti? Shishi hakujali kuchekwa pale alipokosolewa alikubali kujifunza na sasa ameamua kurudi darasani kusoma lugha ili iweze kumsaidia kufika mbali katika mambo yake.

”Mimi nataka nisome kwa furaha yangu mwenyewe ili nijuwe ‘it’s, no’ ‘how am doing, how am speaking’ hicho kitanisaidia sababu kama hela ninazo,” Shishi aliiambia 255 yaxxl kupitia Clouds FM.

“Mimi sitaki kusoma English ili nipate hela cause I have money, nataka tu niweze kurashiarashia hata nikikutana na akina Beyonce nisipate shida.”

ICC Kuzishtaki Uganda na Djibouti kwa Kutomkata Bashir
Video: Kamanda Sirro Azungumzia Sakata la Askofu Gwajima Kukamatwa Airport