Shirika la Viwango Nchini (TBS) liimejipanga kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kumudu ushindani wa masoko ya ndani na nje ya nchi ili kutimiza malengo ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Prof. Egid Mubofu wakati wa mahojiano maalumu katika kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo amesema kuwa, jukumu la nchi kuingia kwenye uchumi wa viwanda si la TBS pekee bali ni la watanzania wote.

“TBS imekuwa na majukumu mbalimbali ikiwemo kuandaa viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa, kutoa elimu kwa wazalishaji wa viwandani ili kusaidia kuzalisha viwango vinavyohitajika na kuhakikisha bidhaa hizo zinakidhi viwango” amesema Prof. Mubofu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Katika kutekeleza malengo hayo, TBS ina mkakati wa kutengeneza ‘Electronic Signature’ itakayowezesha walaji kuhakiki bidhaa iwapo zimekaguliwa kwa kutumia simu ya mkononi kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi.

 

Kesi ya Kitilya na wenzake yazidi kuota mbawa
Simba yazifuata pointi tatu za ubingwa FIFA