Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo jioni kitafanya mazoezi ya mwisho mjini Morogoro, kabla ya kuivaa Mtibwa Sugar kesho Jumamosi (Januari 22), Manungu Complex Wilayani Mvomero.

Simba SC iliwasili jana usiku mjini Morogoro, ikitokea Dar es salaam, na imeweka kambi mjini humo kabla ya kuendelea na Safari ya kuelekea Manungu, ambako mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar utachezwa.

Mchezo huo utazikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza Uwanja wa Manungu Complex, baada ya miaka 22 kupita, ambapo kwa mara ya mwisho Mbungi lilipigwa uwanjani hapo msimu wa 1998-1999.

Simba SC ilisusia mchezo huo kipindi cha pili, ikiwa nyuma kwa mabao 3-1.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 24, huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 12 kwa kumiliki alama 11.

Vlahovic aikataa Arsenal, kusajiliwa Juventus
Nani kuchukua nafasi ya Naibu spika