Simba imetangaza kujitoa kwenye mshindano ya Kagame yanayotarajiwa kufanyika mapema Agosti jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa timu ya Simba, Abbas Ally amesema hawashiriki Kagame ili kutoa nafasi kwa wachezaji kupumzika.

“Tumetoka kwenye Ligi ya Mabingwa halafu tukaunganisha kucheza Ligi Kuu na sasa tumemalizia Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kishindo kwa kutwaa ubingwa dhidi ya watani wetu.”

“Wachezaji wanahitaji mapumziko hata kama ni kwa muda mfupi lakini itawasaidia kuweka miili sawa.”

“Baada ya siku 10 za mapumziko watarejea kambini,” amesema Abbas.

Simba SC imerejea leo Jumatatu (Julai 26) ikitokea Kigoma, baada ya kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC) kwa kuifunga Young Africans bao 1-0 jana Jumapili (Julai 25) Uwanja wa Lake Tanganyika.

Morrison awa kivutio Airport Dar
Mediama yamtema Zana Coulbaly