Jarida la habari la Bild la nchini Ujerumani, limefichua siri ya mazungumzo yaliyokua yakiendelea kati ya uongozi wa mabingwa wa Bundesliga (FC Bayern Munich), na aliyekua meneja wa Arsenal ya England Arsene Wenger.

Jarida hilo limeeleza kuwa, Wenger alianza mawasiliano na uongozi wa FC Bayern Munich kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuwa meneja mkuu, kufuatia mwenendo mbaya wa meneja wa Niko Kovac, ambaye tayari ameshatimuliwa klabuni hapo.

Meneja huyo kutoka Ufaransa aliwasilisha ombi lake kwa mwenyekiti wa FC Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge, kufuatia matokeo mabaya yalowafika The Bavarians mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Eintracht Frankfurt, walioibuka na ushindi wa mabao matano kwa moja.

“Arsene Wenger alimpigia simu Karl-Heinz Rummenigge juzi Jumatano, kwa nia ya kumuomba nafasi ya kuwa meneja mkuu wa kikosi, kufuatia fununu za kutaka kutimuliwa kwa Kovac,” limeleza jarida la Bild.

“Uongozi wa Bayern Munich umekiri kufurahishwa na uwezo wa Arsene Wenger tangu alipokua na kikosi cha Arsenal ya England, lakini umesisitiza kutokua tayari kufanya naye kazi kama meneja mkuu wa kikosi chao.”

Kocha Hansi Flick ambaye alikua msaidizi wa Joachim Low kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani, anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Nico Kovac.

Vyama vya ushirika vyakosa ubunifu utatuzi kero za wakulima
Serikali kutoa elimu ya ujasiriamali kwa walemavu

Comments

comments