Imeelezwa kuwa licha ya juhudi za serikali kusisitiza wakulima kuvitumia vyama vya ushirika kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii bado wameshindwa kubuni mfumo madhubuti wa kuwaunganisha katika ununuzi wa pembejeo ambazo zingewapunguzia gharama za uzalishaji.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS) kwa wenyeviti na mameneja wa vyama vikuu vya ushirika wa kahawa, tumbaku, chai, miwa na mazao mchangayiko yaliyofanyika Jijini dodoma.

Serikali kutoa elimu ya ujasiriamali kwa walemavu

Amesema pamoja na mafanikio ya ushirika ya kutatua changamoto za kiuchumi za wanachama wake na wakulima bado kumekuwa na changamoto za bei ghali za upatikanaji wa pembejeo kutokana na vyama vya ushirika kukosa ubunifu chanya.

“Pamoja na kwamba sera ya maendeleo ya ushirika ya mwaka 2002 inasisitiza kuwa ushirika ni chombo pekee cha kumletea mwananchi mnyonge maendeleo ya kiuchumi na kijamii bado kuna gharama kubwa za upatikanaji wa mbolea,” amefafanua Waziri Hasunga.

Ameongeza kuwa Serikali imeanzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement System – BSP) kupitia kanuni za Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (Fertilizer (Bulk Procurement) ya sheria ya mwaka 2017 ambayo itamsaidia mkulima kupiga hatua na kupata punguzo la bei.

Waziri Hasunga amesema pamoja na kwamba BPS inawalenga zaidi wakulima bado kuna changamoto kwa wakulima wadogo kupitia vyama vyao vya ushirika kutoshiriki kwani tangu kuanza kwa mfumo huo mwaka 2017 uagizaji wa mbolea umekuwa ukifanywa na wafanyabiashara wakubwa pekee.

“Wafanyabiashara hawa wanapoifikisha mbolea kwa wakulima na kukuta hawana fedha hulazimika kuwekewa dhamana za mikopo na wanunuzi wa mazao au wenye viwanda vya mazao ya kilimo ili wapate mikopo ya benki yenye riba kubwa kwa asilimia 15 hadi 20,” ameongeza Hasunga.

Hata hivyo amesema gharama za usambazaji mbolea nchini ni kubwa ikilinganishwa na ile ya uingizaji, jambo ambalo lilisababisha wakulima wadogo kupata mbolea kwa bei kubwa kutokana na wafanyabiashara kutaka faida, riba za mabenki na mifumo ya uingizaji wa mbolea nje isiyo na uwazi.

“Zabuni ya uingizaji wa mbolea aina ya urea kupitia BPS iliyofanyika Julai 04, 2019 bei ya mbolea katika chanzo ilikuwa dola 275 na bei ya kusafirisha baharini na bima ilikuwa dola 29 kwa tani 1 sasa hii ilifanya gharama ya kufikisha mfuko mmoja wa mbolea bandari ya Dar es salaam iwe shilingi 34,500,” amebainisha Hasunga.

Aidha Waziri Hasunga amesema wakati wa ufunguaji wa zabuni kupitia BPS uliofanyika Juni 21, 2019, bei ya mbolea ya kupandia (DAP) iilkuwa kubwa katika soko la Dunia kwa usd 350 – 380 na bei ya mbolea aina za NPK ilikuwa ndogo kea usd 265 – 300.

Kufuatia hali hiyo Waziri Hasunga ameagiza Vyama vikuu vya ushirika kuratibu ukusanyaji wa mahitaji ya mbolea kutoka kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwa wakati na kutathmini gharama zitakazohitajika na kwamba vyama vikuu vya ushirika vihakikishe vinatunza kumbukumbu sahahi za mahesabu ili hati za ukomo zitolewe kwa wakati.

Don Garber: AC Milan inamuwinda Zlatan Ibrahimovic
Siri ya Arsene Wenger kwenda FC Bayern Munich yafichuka

Comments

comments