Mshambuliaji kutoka Burkina Faso na Klabu ya Young Africans Yacouba Sogne amewahakikishia Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, kwa kusema Kiungo Mshambuliaji wa ASEC Mimosas Stephen Aziz Ki atasajiliwa klabu hapo kwa msimu ujao.

Usajili wa Aziz Ki ameleta mkanganyiko mkubwa kufuatia taarifa zake kuhusishwa na klabu nguli za Tanzania Simba SC na Young Afrcans, huku kila upande ukitamba kumnasa katika kipindi hiki.

Sogne ambaye ni raia wa Burkina Faso amesema, amekuwa na mawasiliano na Aziz Ki na amemthibitishia atajiunga na Young Africans kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa.

“KI Aziz amenambia anakuja hapa Young Africans, nina uhakika atakuwa nasi msimu ujao amenihakikishia hilo, atamalizia msimu tu kule atakuja,” amesema Yacouba.

Juzi Jumatano (Juni 15) usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Sogne alitinga uzi wa Aziz Ki, kama sehemu ya kuthibitisha kuwa na uhusiano wa ukaribu kiungo huyo.

Simon Msuva azianika Simba SC, Young Africans
Kocha Mbeya City ataja sababu za kuangusha Point Ligi Kuu