Kocha Mkuu wa kikosi cha Timu ya Taifa ya England Gareth Southgate anatarajia kuanza kufanya mazungumzo na Uongozi wa Chama cha Soka nchini humo, ambayo yatamuwezesha kusaini mkataba mpya wa kuendelea na kazi yake.

Southgate amekua kocha wa kipekee nchini England aliyopa mafanikio timu ya taifa ya nchi hiyo, kwa kufika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2018 na kutinga Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2020 (Euro 2020).

Kocha huyo mzawa amesema anatarajia kuingia kwenye mzungumzo ya kusaini mkataba mpya, baada ya kukamilisha mpango wa kuipeleka England kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2022, zitakazounguma nchini Qatar.

“Nakumbuka nilisema mwezi uliopita kwamba, nimeomba mazunguzo ya mkataba mpya yasongezwe mbele, kwani kwa sasa akili yangu ipo kwenye mechi zilizobaki za kufuzu,” alisema Southgate.

“Baada ya Euro kumekuwa na mzigo mkubwa na kuchoka kutokana na mashindano yale. Nataka kuhakikisha kwamba, ninafanya maamuzi sahihi.”

“Tuna furahi kwamba, tunaongoza kundi kwa sasa. Mazungumzo yapo wazi, lakini si kwa sasa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa FA (Mark Bullingham) amekuwa na sapoti kubwa kwangu.” amesemaq kocha Southgate

England inaongoza kwa tofauti ya alama tatu katika msimamo wa Kundi I, baada ya mchezo wa jana Jumanne (Oktoba 12) dhidi ya Hungary uliomalizika kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London.

Michezo ilioyosalia kwa England kupitia Kundi I ni dhidi ya Albania na San Marino itakayounguruma mwezi Novemba.

Giroud amsubiri kwa hamu Ibrahimovic
Mazungumzo ya kuunda serikali yafikia pazuri Ujerumani