Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameingia rasmi kwenye ‘moyo’ wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikiwa ni miezi michache baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amempendekeza Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho (CC) na kupitishwa na wajumbe wote wa kamati hiyo.

Mbowe alieleza kuwa amefanya uamuzi huo kwa lengo la kuongeza nguvu zaidi na kukiimarisha chama wakijipanga kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2020.

Akizungumza baada ya kupata ridhaa ya kuwa mjumbe wa CC ya Chadema, Sumaye amemshukuru Mbowe na wajumbe wote na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu na utashi wake wote.

Sumaye alitangaza kuikacha CCM miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu na kuunga mkono upande wa vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa na mgombea wake Edward Lowassa.

Picha: Magaidi wa ISIS wawaua mashabiki wa Real Madrid Kikatili
TANZANIA YANG’ARA MKUTANO WA KUPAMBANA NA RUSHWA LONDON

Comments

comments