Mawaziri wakuu wa zamani ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Fredrick Sumaye, jana wamemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema katika Gereza Kuu la Kisongo

Lowassa akiongozana na Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika katika gereza hilo.

“Watanzania wana matumaini makubwa sana na mahakama, wanaamini chombo hiki pekee ndicho kitakachowapa haki yao, hivyo kwa mwaka 2017 mahakama itoe haki na kuendesha kesi bila upendeleo kwa sababu ndiyo sauti ya wanyonge, nakutakia amani na mwaka mpya mwema,” Calist alimnukuu Lowassa.

“Nimemwachia ujumbe ‘just be strong’ (awe jasiri), haya yote yatapita muda wake ukifika, suala lake liko mahakamani sio la kisiasa, hata kama lililomleta huku linahusiana na siasa, suala la dhamana tunatarajia litafika mwisho wake, lakini nimemwambia hata kama dhamana ikikosekana, bado kesi ya msingi itafika mwisho wake, asiwe na wasiwasi wala hamaki, awe jasiri asikate tamaa,” alisema Sumaye.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka jana akiwa nje ya Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kufikishwa mahakamani Novemba 11, mwaka jana akikabiliwa na kesi za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli na hadi wakati huu bado anashikiliwa mahabusu katika gereza hilo.

Mwanafunzi wa Sekondari auawa kwa risasi
Majaliwa awaagiza waalimu kuishi karibu na shule wanazofundishia