Idadi ya ajali za barabarani Tanzania inazidi kupamba moto, takwimu zinaonyesha kuanzia januari hadi juni ni zaidi watu 1580 wamepoteza maisha katika ajali tofauti tofauti, sawa na wastani wa watu tisa wanakufa kila siku.

Mnamo Julia Mosi, 2016 watu 11 walipoteza maisha na wengine 44 kujeruhiwa baada ya magari matatu kugongana eneo la Dumila Morogoro, Pia mnamo Julai 5, 2016 watu 30 walifariki dunia baada ya mabasi ya City Boy kugongana katika eneo la Maweni mkoani Singida na kusababisha majeruhi 48, pia usiku wa kuamkia juzi watu 12 walifariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa baada ya basi la New Force  likitokea Dar es salaam kwenda Songea kupinduka katika kijiji cha Lilombwi Tarafa ya Igominyi na pia juzi kuamkia jana ajali nyingine ilitokea kati ya daladala iliyokuwa ikitokea kijiji cha Shilima kwenda Nyegezi na basi la Super Shem lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza ambapo watu 13 walifariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa.

Kufuatiwa ajali hizo Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kupatwa hofu juu ya ajali na vifo vilivyojitokeza,  hivyo Serikali ipo katika hatua za mwisho kupanga mkakati wa kuanzisha kitengo  cha kupima madereva ili kubaini aina ya vilevi wanavyotumia.

Ajali zinazotokea barabarani mara nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva, sheria zimewekwa zifuatwe  lakini kutokana na mapuuza ambayo madereva wengi wanayo wanafanya kama sheria zimewekwa zivunjwe, kwa taarifa hiyo fupi inaonesha ajali nyingi zinasababishwa na madereva wa mabasi ya kusafirisha abiria.

Sheria thabiti inabidi ifanye kazi yake kuhakikisha ajali hizi zinapungua.

Hili ni tatizo kubwa kwa nchi kwani vifo vya ajali ni vifo vinavyoweza kuzuilika, na kuzuilika kwake ni kwa kufuata sheria za barabarani, elimu inayotolewa kwa madereva isisitize sana ufuataji wa sheria za barabarani ili kuepusha ajali.

 

Wazo la leo juu ya mafanikio.
Asilimia 80 ya walimu shule za msingi Uganda hawajui kusoma

Comments

comments