Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) inaandaa utaratibu wa kukata rufaa dhidhi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), William Mhando, mkewe Eva Mhando na wenzake.

Uamuzi huo wa Takukuru ulitangazwa jana na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo, Tunu Mley ambaye alisema hawakuridhika na uamuzi wa Mahakama hiyo, hivyo kwa mujibu wa sheria wanakata rufaa katika Mahakama ya juu zaidi ambayo ni Mahakama Kuu.

Takukuru wamefikia hatua hiyo ikiwa ni saa kadhaa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaachia huru baada ya kuona kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka haukuwa na mashiko ya kuwatia hatiani washtakiwa.

Mhando, mkewe Eva na wenzake walikuwa wakishtakiwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na udanganyifu. Mhando alidaiwa kutumia nafasi yake kuipatia zabuni kampuni anayoimiki yeye, mkewe na mwanae, kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma.

Hata hivyo, Mahakama hiyo haikumtia hatiani Mhando na kueleza kuwa Mhando hakuwa anaingia kwenye vikao vya Bodi ambavyo vilikuwa vinatoa maamuzi ya zabuni hivyo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa alishawishi kampuni yake kupewa zabuni husika.

Bunge laja kivingine, Vyombo vya habari kupata matangazo yake bila kufunga mitambo Bungeni
Klopp: Ni Marufuku Kushika Nembo Ya Klabu Ya Liverpool