Tani 622.4 za sukari zimekamatwa mkoani Morogoro zikiwa zimefungiwa kwenye magodauni mbalimbali ya wafanya biashara katika wilaya za Kilombero,Kilosa pamoja na Morogoro ambapo Mkuu wa Mkoa huo Dr Stephen Kebwe amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa kuweka ulinzi kwenye maghala hayo na kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Tani hizo za sukari zimepatikana baada ya Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dokta Stephen Kebwe kufanya msako mkubwa wa kubaini wafanyabiashara walioficha sukari kwa lengo la kuhujumu uchumi ambapo mkuu huyo wa mkoa amesema atahakikisha sukari yote iliyofichwa inapatikana na kuuzwa kwabei elekezi ya serikali.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakihojiwa na ITV wameeleza kusikitishwa na hatua ya sukari kukosekana ghafla na kupanda bei mara mbili ilivyokuwa inauzwa licha ya mkoa wa Morogoro kuongoza kwa kuwa na viwanda vingi vya sukari kuliko mikoa mingine ambapo wameiomba serikali kuwachukulia hatua madhubuti wafanyabiashara waliotumia fursa hiyo kuhujumu uchumi wa  nchi.

Tani 622.4 za sukari zimekamatwa mkoani Morogoro zikiwa zimefungiwa kwenye magodauni mbalimbali ya wafanya biashara katika wilaya za Kilombero,Kilosa pamoja na Morogoro ambapo Mkuu wa Mkoa huo Dr Stephen Kebwe amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa kuweka ulinzi kwenye maghala hayo na kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Tani hizo za sukari zimepatikana baada ya Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dokta Stephen Kebwe kufanya msako mkubwa wa kubaini wafanyabiashara walioficha sukari kwa lengo la kuhujumu uchumi ambapo mkuu huyo wa mkoa amesema atahakikisha sukari yote iliyofichwa inapatikana na kuuzwa kwabei elekezi ya serikali.

Msichana aliyebakwa na baba yake aambulia kuchapwa bakora na wanakijiji
Kigwangalla amtaka Gardner kuomba radhi kwa kauli chafu dhidi ya Lady Jaydee