Serikali ya Tanzania imeendelea kushirikiana na nchi Jumuiya za Umoja wa Afrika katika kuendeleza utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi wanachama.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani 2021 yaliyofanyika Jijini Abidjan nchini Côte d’ Ivoire leo.

“Lengo kuu la kushiriki katika Maadhimisho haya ni kujifunza na kuangalia namna ya kendeleza utalii wetu hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na janga Uviko 19 lililoikumba dunia,” Amesema Naibu Waziri Masanja.

Aidha, Naibu Waziri Mary Masanja amesema kuwa ushiriki huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu lakini pia kuvitangaza vivutio vya Utalii vilivyoko nchini Tanzania ikiwa ni moja ya juhudi za kuunga mkono kazi anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii duniani.


Tanzania huadhimisha Siku ya Utalii Duniani kila mwaka Septemba 27 na kauli mbiu ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka huu ni “Utalii kwa Maendeleo Shirikishi/ Jumuishi

Korea kusini yapiga marufu ulaji wa mbwa
Nyota R. Kelly apatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono