viongozi wa Tanzania na Uganda hatimaye wamekubaliana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka mji wa Hoima nchini Uganda hadi changalieni mjini TangaTanzania.

Katika makubaliano hayo yaliotiwa saini na mawaziri wa nishati kutoka pande hizo mbili na marais wa mataifa hayo mawili John Pombe Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda , asilimia 60 ya faida ya mafuta hayo itaenda kwa Tanzania huku asilimia 40 ikienda kwa Uganda.

Akizungumza katika hafla hiyo , rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kwamba cha muhimu ilikuwa kuanza mradi huo aliodai kucheleweshwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

“Niliamua kwamba wacha tuwache kuchelewesha tuanze mradi. Tuliongea kwa simu mimi na mdogo wangu, nikamwambia achukue hata asilimia 70 au 80 lakini mdogo wangu akaona aibu akasema hapana , ni asilimia 60 itakwenda Tanzania, 40 nayo ikisalia na Uganda,” amesema Mseveni

Awali akizungumza , rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utaimarisha uchumi wa mataifa haya mawili na eneo lote la Afrika mashariki na kati.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 14, 2020
Majaliwa : mamlaka ya maji kuanzishwa Chemba