Ili kuibua fursa zilizopo katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Tanzania inakusudia kuendeleza ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo vyombo vya Habari kufahamu mikakati na malengo itakayofanikisha matokeo chanya.

Balozi, Agnes Kayola ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wanahabari yanayofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine ambayo yameratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).

Baadhi ya Washiriki kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari katika mafunzo ya siku mbili kwa Wanahabari yanayofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani yaliyoanza hii leo Julai 25, 2022.

Amesema, warsha hiyo inalenga kuwajengea uelewa Wanahabari juu ya kazi za SADC, na kushiriki kuiarifu jamii hasa ya Watanzania kuhamasika na kuzitambua fursa zilizopo katika jumuiya hiyo na kuzitumia kikamilifu.

Balozi Kayola amesema, “Tanzania ni nchi mwanzilishi wa SADC yenye umri wa miaka 40 hivyo Waandishi mnatakiwa kuhakikisha kundi la vijana linafahamu umuhimu wa Jumuiya hii ili waweze kushiriki na kuzitumia fursa zilizopo kikanda.”

Nchi wanachama wa SADC katika ramani.

Ameongeza kuwa, katika kufanikisha malengo ya SADC, Serikali itaendelea kutumia lugha ya Kiswahili kama bidhaa, ambayo hivi karibuni imetajwa kuwa moja ya lugha adhimu inayotumiwa na Mataifa mbalimbali Ulimwenguni na kuhimiza Vyombo vya Habari kuendelea kuitumia kifasaha.

Aidha, Balozi pia amesisitiza malengo ya SADC kuwa yanalenga kufikia maendeleo ya kiuchumi, amani, usalama,kupunguza umaskini, kuimarisha kiwango na kuhakikisha uwepo wa maisha bora ya watu wa eneo la ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Bilioni 1.1 zakusanywa kampeni GGM Kili Challenge 2022
James Kotei aongeza miwili Singida Big Stars