Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Januari 22, 2021 katika Hospitali ya Milambo Mkoani Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amethibitisha kifo chake cha Magaga na kueleza kuwa Maganga amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Milambo Tabora, alipokuwa akisumbuliwa na presha na sukari ambavyo vilipelekea moyo kufeli.

“Maganga amefariki kwenye Hospitali ya Milambo, hakulazwa, alikuwa na ujenzi kwenye site yake akaja pale leo usiku amezidiwa, ni presha na sukari ilikuwa imepanda halafu moyo ukafeli, mwili uko mochwari wakati tukiendelea na taratibu nyingine,” amesema Sengati.

Brig.Jen Mstaafu Emmanuel Maganga aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kabla ya kustaafu na nafasi yake kuchukuliwa na Andengenye,.

DPP awafutia mashtaka washtakiwa 57
NEC yajibu vikwazo vya Marekani