Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi alifariki dunia jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk. Makongoro Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.

“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli ingawa jioni hii sijaenda hospitali, ninafanya mawasiliano na familia lakini taarifa kamili kuhusu msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye tutamteua usiku huu, na kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Dk. Mahanga anakaririwa na Mtanzania.

Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Dar24 inatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa msiba huu wa aliyekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa Amani. Amina!

VIDEO: YCEE AUNGANA NA DJ MAPHORISA KUTENGENEZA REMIX KALI YA ‘O’MO ALHAJI
Video: Moladi kujenga nyumba za Watumishi Dodoma