Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoani Manyara, Martha Jachi Umbulla mwenye umri wa miaka 65 amefariki dunia leo Januari 21, 2021 saa saba usiku kwa saa za India.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, kifo cha Mbunge huyo kimetokea katika Hospitali ya HCG Mumbai, Nchini India ambapo alikuwa anapatiwa matibabu.

Kufuatia msiba huo, Spika Ndugai ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza mpendwa wao.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Familia inaratibu mipango ya mazishi.

NEC yajibu vikwazo vya Marekani
Biden airejesha Marekani kwenye ushirika na WHO