Mpiga Picha mkongwe wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, amefariki dunia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Senga alipelekwa nchini humo kwa matibabu ya moyo, ambapo tayari alikwisha ruhusiwa baada ya matibabu na kurejea hotelini kwake kwa mapumziko na kujiandaa na safari ya kurejea nchini.
 
Kabla ya kifo chake imeelezwa kuwa Marehemu alizungumza na mkewe kwa njia ya simu akimueleza kuwa hali yake ni nzuri na anaendelea vizuri na kwamba alitarajia kuanza safari ya kurejea nchini mnamo tarehe 5-8-2016 na alitarajia kufika Tanzania tarehe 6-8-2016.
Hali ya Marehemu ilianza kubadilika jioni ya jana na kurudishwa Hospitalini.
Wakiwa njiani hali yake ilizidi kubadilika na baada ya kufika Hospitalini hapo Madaktari walimpima na kuthibitisha kuwa tayari alikwishafariki dunia.

damer i norge

Video: Papa Francis aanguka ghafla akiongoza Ibada
TFF: Muda Wa Usajili Wa Wachezaji Hautaongezwa