Watu watano wamefariki na wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali mbaya iliyohusisha roli la kubeba mchanga na magari mengine matatu yakiwemo yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati ya Bunge(Utawala na TAMISEMI), katika eneo la Kerege, Bagamoyo Pwani.

Taarifa rasmi imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya roli la mchanga kugonga kwa nyuma gari dogo lililokuwa linatoka Bagamoyo kwenda jijini Dar es Salaam lililopunguza mwendo ghafla.

Baada ya roli hilo kuliganga gari hilo dogo, lilihama na kwenda upande wa pili ambapo liligonga magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo ya Bunge. Magari hayo yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati ya Bunge ni gari la Tasaf na la Mkurugenzi wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Bakabogo.

Waliothibitishwa kufariki katika ajali ni Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara ya Mipango ya Uchumi, Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan (40), Tunsime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya  na Ludovick Palangya, Mchumi.

Majeruhi kumi na mbili wameripotiwa kulazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wote wa Kamati ya Bunge walinusurika katika ajali hiyo.

Magufuli: Wana CCM tusilazimishe Mambo Umeya Dar
Coastal Union Kutangaza Msimamo Wa Kujinusru Kushuka Daraja