Shirika la Viwango Tanzania TBS limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazozagaa mtandaoni kuhusu kinywaji aina ya ukwaji na kukanusha madai kwamba kinywaji hiko kinatengenezwa chini ya ubora kwa kuwekewa kemikali aina ya Benzene.

Kinywaji hiko kinchotengezwa na kampuni ya Bakhresa Food Products kwa sasa ni miongoni mwa vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi zaidi kutokana na radha yake halisi ya ukwaju ambao hufurahisha makoo ya watu.

Hivyo TBS katika taarifa yake imetoa ufafanuzi wa kitaalamu kabisa ikidai kuwa kinywaji cha Ukwaju ni salama kwa afya na kinatengenezwa na kuhifadiwa katika ubora wa hali ya juu, hivyo kimewaomba wapenzi watumiaji wa kinywaji hiko kupuuzia taarifa zilizosambaa kuhusu kinywaji hiko kuwa hakina viwango kutokana na kuwekwa kwa kemikali hiyo aina ya benzene.

TBS imefika mbali zaidi kwa kuthibitisha ubora wa kinywaji hiko kwa kutaja leseni Na. 1159 kuwa ina kiwango cha taifa Na.585:2011.

Vile vile imearifu kuwa vitunzio vya kinywaji hiko ni vitunzio vinavyokubalika na kuruhusiwa kwa mujibu wa viwango na miongozo ya kitaifa na kimataifa.

Hivyo imeomba wananchi kuepuka kutoa taarifa ambazo zinazua taharuki na kupotosha jamii.

Lakini pia shirika  linaendelea kufuatilia wazalishaji na wasambazaji mbalimbali wa bidhaa ili kuhakikisha kanuni na taratibiu za usalama na ubora zinazingatiwa.

 

 

Malawi: wanafunzi watetewa na Mahakama kusokota ''dread'' shuleni
Serikali yaagiza Chuo cha Diplomasia kutoa elimu ya vitendo

Comments

comments