Klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21 zimetakiwa kuwasilisha wasifu na vyeti vya makocha wao.

Ombi hilo kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, limetolewa na Shirikisho la soka nchini TFF, leo Septemba 10, kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino inyoongozwa na Cliford Ndimbo.

Ndimbo amezungumza na waandishi wa habari leo mchana na kusema klabu za Ligi Kuu Bara, zinapaswa kuwasilisha TFF wasifu na vyeti vya makocha wakuu, Makocha wasaidizi, Makocha wa viungo na Makocha wa makipa.

Amesema mwisho wa kuwasilisha wasifu na vyeti Septemba 15, 2020 na vitu hivyo vinatakiwa kukabidhiwa  kwa mkurugenzi wa ufundi TFF Oscar Mirambo.

Tamko hilo limetolewa ikiwa na lengo la kuzikumbusha klabu kutekeleza kanuni na sheria za TFF kukusanya taarifa za viongozi na makocha wa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Kilimo cha mbogamboga kukuza uchumi wa Tanzania
Basi la Isamilo lapata ajali Mbeya