Mamlaka  ya Usimaizi Bandari nchini (TPA), imesema ipo katika maandalizi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, itakayosaidia utoaji wa huduma za upakiaji na kushusha mzigo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa wakati akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), waliofika kutaka kujua mipango mbalimbali ya mamlaka hiyo katika kuboresha utoaji wa huduma.

Picha ikionesha mfano wa ujenzi Bandari ya Bagamoyo.

Amesema, kuanzia Januari mwaka 2023 TPA itaanza ujenzi wa kituo kikubwa cha kisasa cha kupokelea mafuta katika bandari ya Dar es Salaam, hatua itakayosaidia  meli kutotumia muda mrefu kushusha mzigo.

Awali  Mwenyekiti wa Bodi ya EABC, Anjelina Ngalula, alisema yeye pamoja na wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wako tayari kutumia bandari ya Dar es Salaam katika kushusha mizigo yao, kwa kuwa malalamiko yaliyokuwepo awali yamefanyiwa kazi.

Nini kitatokea ikiwa Putin atatumia silaha za Nyuklia?
China na India zaonesha dalili 'kuipotezea' Urusi