Mtoto mmoja amefariki dunia huku watu watano wakijeruhiwa baada ya treni ya abiria kupata ajali katika eneo kati ya Mkalamo na Mvave Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk imesema kuwa Treni ya abiria iliyokuwa inatoka Arusha kwenda Dar es Salaam, yenye injini namba 9022 imepata ajali majira ya saa 10 alfajiri kati ya Mkalamo na Mvave wilaya ya Pangani mkoani Tanga Januari 16, 2022.

TRC imesema kuwa treni hiyo ilitoka Arusha jana Jumamosi mchana kuelekea Dar es Salaam ikiwa na mabehewa 14 yaliyobeba abiria 700 huku mabehewa matano yakipinduka.

“Ilipofika eneo lililopo kati ya Mkalamo na Mvave (km 88) behewa 5 zilipinduka na nyingine 4 kuacha njia na kupelekea majeruhi 5 ambapo wanaume ni 3 na wanawake 2 na kifo cha mtoto Hassan Lugano mwenye umri wa miaka 7.

Taarifa hiyo imesema majeruhi tayari wamepelekwa katika Zahanati ya Mkalamo kwa ajili ya kupatiwa maatibabu na wanaendelea vizuri huku Shirika likiendelea na taratibu nyingine kurejesha huduma za usafiri.

“Shirika la Reli linaendelea kufuatilia kwa karibu kufahamu chanzo cha ajali ili kuchukua hatua, aidha Shirika linatoa pole kwa familia ya marehemu na linawaombea rnajeruhi we ajali wapate nafuu maperna iii waweze kuendelea na majukurnu ya kujenga Taifa.” Imesema taarifa hiyo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 17, 2022
'Mzee wa Nyororo':Maneno ya DP Ruto yamkera Francis Atwoli